Kiwanda cha Vigae Mkuranga Kupatiwa Gesi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Mdini Prof. Justin Ntalikwa (aliyevaa shati la kitenge) akioneshwa na Kaimu Mkurugenzi Mtaendaji wa Kampuni ya Goodwill, Robin Huang (aliyenyoosha mkono kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtaendaji wa TPDC (aliyenyoosha mkono kulia) eneo patakapo jengwa bomba la kuunganisha gesi katika kiwanda cha Goodwill cha kuzalisha vigae Wilaya ya Mkulanga Mkoani Pwa

 

Kaibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa amesema kuwa serikali itaunganisha kuunganisha gesi asilia katika kiwanda cha vigae kilichopo Wilaya ya Mkuranga, Mkoani Pwani.

Alisema kiwanda cha Kampuni ya Goodwill inayoendelea na ujenzi wa Kiwanda hicho itaunganishiwa gesi na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) mara baada ya ujenzi kukamilika.

“Kiwanda hiki kinatarajia kuzalisha vigae kwa ajili ya shughuli mbali mbali za ujenzi na katika kuzalisha vigae hivyo Kampuni itahitaji gesi kwa ajili ya kuendesha mitambo na kuzalisha umeme wa megawati nane (8) kwa ajili ya kuendeshea kiwanda, alisema Prof. Ntalikwa.

Alisema kuwa kwa upande wa Wizara ya Nishati na Madini itahakikisha gesi inayohitajika wanapatikana, ili kutowakwamisha katika juhudi zao za uzalishaji.

“Sehemu ambayo gesi itaunganishwa iko karibu ni umbali wa chini ya kilomita moja, kwa maana hiyo kazi iliyopo nikujenga bomba dogo litakalo unganishwa na bomba kubwa la TPDC la nchi thelathini na sita (36),” alifafanua Ntalikwa.

Prof. Ntalikwa alisema kuwa ujenzi wa Kiwanda unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu na zao la kwanza la kiwanda linatarajiwa kutoka mwezi januari mwakani.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba alisema TPDC ikotayari kuona Serikali inafanikiwa katika malengo ya kuwa na viwanda na gesi inakuwepo kwa viwanda hivyo.

“Tumekuwa na mazungumzo mazuri na Kampuni ya Goodwill kwa ajili ya kuwaunganishia gesi katika Kiwanda chao na hatuo iliyopo ni kujenga bomba la kuunganishiwa gesi hiyo,” alisema Mhandisi Musomba.

Aliongeza kuwa Kiwanda cha Goodwill ni kiwanda cha kwanza kwa upande wa TPDC ambacho ndicho kitauziwa gesi ukiondoa Tanescio ambayo imekuwa ikiuziwa.

Aidha, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Goodwill, Robin Huang alisema kuwa matumizi ya nishati ya gesi asilia ni nafuu katika uendeshaji wa kiwanda.

“Tutatumia gesi asilia kama nishati kuu kwa ajili ya uzalishaji katika kiwanda chetu kwani ni nafuu kwa bei na tumepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Serikali” alisema Huang.

Gesi itakayo hitajika katika kiwanda hicho kwa kuanzia itakuwa futi za ujazo milioni 7 kwa siku, na baada ya miaka mitatu itafikia futi za ujazo milioni 10 kwa siku.

Kiwanda cha Goodwill kinatarajia kukamilika ujenzi wake mwezi Disemba na kuanza uzalishaji mwezi Januari 2016. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha mita za maraba 8,000 kwa siku.

Uzalishaji wa kiwanda hicho unategemea kuchukua sehemu kubwa ya soko la vigae vya ujenzi nchini, kwani kinatarajiwa kufungua matawi katika miji yote mikubwa chini.


Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *